NAIBU MEYA MASABURI AWATAKA WANANCHI CHANIKA KUMPIGIA KURA DKt SAMIA


NAIBU MEYA wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam ambaye ni Diwani wa kata ya Chanika Wilayani Ilala Ojambi Masaburi amewataka wananchi wa kata ya Chanika kumpigia kura Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan pamoja na  Mgombea mweza nafasi ya Makam wa Rais Dkt. Emanuel Nchimbi  .

Naibu Meya Ojambi Masaburi, alisema hayo kata ya Chanika Wilayani Ilala wakati wa  uzinduzi wa shirika lisilo la kiserikali la Mulika Community Organization Tanzania linaloshugjulikia maswala ya kijamii yakiwemo ya vitendo vya ukatili. 

"Wananchi wangu wa Chanika Wilayani Ilala kula zote kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan amefanya makubwa kata ya Chanika na Wilaya yetu ya Ilala ambapo kwa Chanika baadhi ya mambo aliyoyafanya kituo cha mabasi ya kisasa kinaenda kufunguliwa ,soko la kisasa linajengwa   sekta ya Elimu ameongeza madarasa ya elimu msingi na sekondari pamoja na kituo cha afya cha kisasa  "alisema Masaburi  

Masaburi alisema Rais Dkt.Samia amefanya makubwa hivyo yeye na wananchi wake wanamuunga mkono kwa kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo ikiwemo mradi wa maji ya DAWASA wa Bangulo hivi karibuni maji yatafika Chanika. 

Akizungumzia  miundombinu ya barabara alisema kilometa 72 barabara zimejengwa Ukonga kwa kiwango cha lami maji safi na Salama yanaingia Chanika. 

Aliwataka wananchi wajiepushe na makundi badala yake amewataka kuunga mkono juhudi za Rais Dkt.Samia za kuleta maendeleo na kusimamia miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na Rais ikiwemo Reli ya kisasa SGR ,Bwawa la Mwalimu Julius Nyerere   sekta ya afya na sekta ya Elimu pamoja na miundombinu ya Barabara zote ni juhudi za Serikali ya awamu ya sita. 

Katika hatua nyingine aliwatka Watanzania kuishi kwa Amani na Upendo kwa kudumisha umoja na mshikamano nchi yetu isiingie katika vita sio vizuri 

Akizungumzia kugawa Jimbo la Ukonga kuzaa jimbo la Kivule alisema yaliopelekwa ni ushauri na mapendezo   kutokana na jimbo hilo kuwa na idadi ya wananchi wengi zaidi ya 900 000 hivyo mapendekezo hayo bado kufanyiwa kazi.

"MImi Ojambi Masaburi Diwani wa Kata ya Chanika nimefanya kazi kubwa ya utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi kwa kuwatumikia wananchi wangu naendelea na nafasi yangu ya Diwani wa Kata ya Chanika   kwa ajili ya kutumikia wananchi wangu"alisema Masaburi.

Comments