DIWANI AISHA JOHARI ATOA KADI ZA BIMA YA AFYA KWA MAKUNDI MAALUM


DIWANI wa Viti Maalum Wanawake wilaya ya Ilala Aisha Johari,  ametoa kadi za Bima ya afya kwa watoto wa Makundi Maalum kata ya Liwiti wilayani Ilala ,ili ziweze kuwasaidia katika   matibabu. 

Diwani Aisha Johari, alitoa msaada huo wa kadi za Bima ya afya mtaa wa Misewe kata ya Liwiti  Dar es Salaam leo kwa watoto wa mahitaji Maalum watatu sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi. 

Akikabidhi kadi hizo pamoja na viongozi wa umoja wanawake UWT kata ya Liwiti Johari aliwataka  Wazazi wa Watoto hao kuzitumia bima ya afya hizo zilizoboreshwa katika vituo vya afya vya Serikali  .


"Leo nimekabidhi kadi za bima ya afya kwa watoto wa mahitaji maalum kata ya Liwiti pamoja na viongozi wa Umoja wanawake UWT awali nilipokea changamoto hii kupitia UWT leo nimekuja kutekeleza "alisema Johari. 

Diwani Johari alisema anaunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kusaidia jamii upande wa sekta ya afya katika suala zima la matibabu kusaidia watoto wa makundi maalum waweze kupata huduma za afya.

Aidha aliwataka wananchi kusaidia watoto wa makundi maalum katika masuala mbali mbali ya elimu na afya ili waweze kufurahi kama jamii nyingine .

Alisema yeye ni Diwani wa Viti Maalum wilaya ya Ilala anasaidia wilaya ya Ilala nzima kutatua changamoto mbalimbali za wananchi. 


Katibu wa UWT Liwiti Habiba Rajabu alimpongeza Diwani Johari sehemu ya msaada aliotoa wa bima ya afya kwa wananchi.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Misewe Kata ya Liwiti Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Said  Badri Matossa alisema katika mtaa wake kuna watoto wa mahitaji Maalum zaidi 15  amewataka madiwani wengine ,wananchi kuweka utaratibu wa kutembelea watoto wa makundi maalum kwa ajili ya kuwasaidia. 

Comments