HOSPITALI YA RUFAA YA AMANA WAPATA TUZO YA HUDUMA BORA


HOSPITALI ya Rufaa ya Mkoa Amana Serikali imewapa tuzo ya huduma bora ya MatibabuTanzania katika hospitali 28 za Rufaa Amana imekuwa kinara na kushika namba moja.

Akizungumza katika hafla fupi hospitalini hapo Katibu Tawala wa Mkoa Dar es Salaam Toba Nguvila,alianza kwa kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan ,kwa kazi kubwa katika kuboresha miundombinu ya sekta ya afya nchini na mkoa wa Dar es salaam.

"Hospitali yetu ya Rufaa ya Mkoa Amana inafanya kazi kubwa  Dkt, Brayson Kiwelu amefanya makubwa katika kuisimamia  sekta ya afya hospitali yetu ya Amana inatoa mchango mkubwa kuisaidia Serikali kupitia Mganga mkuu amekuwa mbunifu wa mikakati mbali mbali kwa ajili ya kuiendeleza hospitali hii na sasa malalamiko yamepungua kwa wagonjwa hospital ina vifaa bora ,wauguzi bora " alisema Toba.


Katibu Tawala Mkoa alisema kwa sasa Amana ina madaktari bingwa wa kisasa,wauguzi bora na vifaa vya kisasa hivyo tujivunie ni matunda ya Serikali ya Dkt.Samia Suluhu Hassan kwenye sekta ya afya Waziri alitoa tuzo hiyo Aprili 8 mwaka huu kwa niaba ya Rais .

Alisema katika mafanikio apakosi changamoto kuhusiana na changamoto za eneo la upanuzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana eneo la NHC la Shirika la Nyumba ambalo mmeomba  atawasilisha kwa Mkuu wa Mkoa Albert John Chalamila, ili waweze kuliomba eneo hilo wabadilishe matumizi , kuhusiana na changamoto za bima ya afya amelichukua pia atawasilisha Ofisi ya mkoa.

Mganga mfawidhi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana Wilayani Ilala, Brayson Kiwelu alisema ameshukuru Wizara ya afya kwa mafanikio makubwa ikiwemo jitihada za watumishi wake wa Amana kupitia umoja wao wamekuwa wakifanya vizuri ngazi ya mkoa katika hospitali hiyo. 

Dkt Brayson Kiwelu alisema mwaka jana waliandaa siku ya chakula cha usiku kwa ajili ya kuchangia maboresho ya Miundombinu ya Amana na sasa wanaendelea kuboresha hutoaji huduma bora aprili 8 mwaka huu walikuwa na kikao cha Bodi wakapata tuzo hiyo ngazi ya Kitaifa sasa wanajipanga waweze kuchukua ngazi ya kimataifa alitumia fursa hiyo kumshukuru Rais Dkt.Samia na kumpongeza kwa jitihada zake kubwa kuisimamia sekta ya afya vizuri.


Mjumbe wa Bodi ya hospitali ya mkoa Amana Idda Luhanga ,alitoa pongezi za dhati kwa Wafanyakazi na watumishi wa Amana kwa niaba ya Watoto Njiti na wagonjwa wote wanaopata matibabu Amana 

Mjumbe Idda Luhanga alisema mikakati yao wachukue tuzo zote kila mwaka katika hospitali hiyo watachukua  maoni ya wateja kupitia sanduku la  maoni.

Comments