Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imepokea timu ya wataalamu kutoka Ofisi za Umoja wa Afrika (AUC) wanaoratibu utekelezaji wa mradi wa kuboresha huduma za hali ya hewa wa “Intra-ACP Climate Services and related Applications Programme (ClimSA)”.
Ziara
hiyo ilifanyika tarehe 17 Aprili, 2025 ikioongozwa na mmoja wa
Wasimamizi wa mradi wa ClimSA kutoka AUC Bw. Freddy Falanga (ambaye ni
rai wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo), ambapo timu hiyo ya wataalamu
walitembelea Ofisi Kuu ya Utabiri wa Hali ya Hewa, iliyopo Ubungo Plaza,
Dar es salaam kwa lengo la kukagua utendaji kazi wa mitambo ya
ufuatiliaji wa mifumo ya hali ya hewa na utabiri wa hali ya hewa,
inayoitwa "PUMA STATION.", iliyotolewa kwa TMA kupitia mradi ClimSA.
Mradi
wa ClimSA unatekelezwa katika nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AUC),
ikiwemo Tanzania kwa ufadhili wa Umoja wa Ulaya (European Union). Mradi
huu unalenga kuimarisha zaidi uwezo wa nchi wanachama wa AU katika
kufuatilia mifumo ya hali ya hewa kupitia teknolojia ya satelaiti ili
kuboresha zaidi utabiri wa hali ya hewa na huduma za hali ya hewa kwa
ujumla.

Comments
Post a Comment