RC CHALAMILA AMALIZA MGOGORO WA WAFANYABIASHARA WA MANZESE NA HALMASHAURI YA UBUNGO

 


-Awataka kuanzia jumatatu mfanyabiashara mmoja mmoja kuandika maelezo ya kiasi cha ushuru wa huduma anachodaiwa na namna ambavyo ataweza kulipa ili Halmashauri ione namna bora ya wafanyabiashara hao kulipa deni hilo.

-Akemea tabia ya wafanyabiashara kuwa wanaharakati, kila jambo linazungumkika hakuna sababu ya kufunga maduka

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Julai 12,2025 amemaliza mgogoro wa jumuiya ya wafanyabiasha wa Manzese na Halmashauri ya Ubungo ambao umetokana na wafanyabiasha hao kushindwa kulipa Ushuru wa Huduma "Service Levy" ambao ulipelekea wafanyabiasha hao kufunga maduka 11 wakidai Serikali iwatoze ushuru huo kwa "flat rate"


RC Chalamila amesema Serikali chini ya uongozi mahiri wa Dkt Samia Suluhu Hassan inawathamini sana wafanyabiasha na siku zote Rais ameendelea kuweka mazingira rafiki ya kufanya biashara, hivyo kwa kuwa Ushuru wa Huduma uko kisheria ni vigumu kubadili takwa hilo la kisheria kwa sasa ni lazima wizara husika ihusishwe hivyo ni mchakato.

Kwa mantiki hiyo RC Chalamila amewataka wafanyabiasha hao kuandika maelezo ya kuomba kupewa muda maalum wa kukamilisha deni hilo ili timu ya watalaam wa biashara ikae ione namna bora ya wafanyabiasha hao tena mmoja mmoja atakavyoweza kulipa deni hilo bila kuathiri biashara yake.  

Aidha RC Chalamila amekemea tabia ya uanaharakati kwenye  biashara, "migomo haina tija kamwe usidanganyike kuwa katika vikundi kugoma, biashara ni ya mtu mmoja mmoja na sio kikundi " Alisema RC Chalamila 

Mwisho Wafanyabiasha hao wameridhia kufungua maduka yao na sasa wanaendelea na biashara kama ilivyokuwa awali.


Comments