SERIKALI YAPONGEZWA KWA KUIWEZESHA ‘I TRUST FINANCE’ KUANZISHA ‘I DOLLAR’


Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA)
Mhe. Nicodemus Mkama aipongeza serikali kwa kuendelea kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji wa ndani na nje hatimae kuwezesha mamlaka kuweza kutoa idhini kwa I Trust Finance kuanzisha mfumo wa uwekezaji wa ‘I Dollar’.

Pongezi hizo zimetolewa leo Julai 10,2025, Dar es Salaam, katika hafla ya uzinduzi wa Mfuko huo wenye lengo la la kuwekeza fedha za kigeni, ambapo kiwango cha chini cha Uwekezaji ni Dolar 1 na faida inatolewa fedha ya Kigeni hiyo.


“Tunatoa pongezi kubwa sana kwa serikali kwa kuweza kuweka mazingira mazuri ambayo yamewezesha mamlaka kuweza kutoa idhini kwa I Trust Finance kwa kuanzisha mfuko wa kwanza ambao unatoa fursa kwa wawekezaji wa Kitanzania kuwekeza katika fedha za Kigeni (Dollar).”

“Hii ni fursa nzuri kwa Watanzania kuweza kuhakikisha kwamba wanaweza kuwekeza kwa njia ya fedha za kigeni (dollar), tuna toa rai kwa wawekezaji wote wa Kitanzania ikiwaq ni Pamoja na mtu mmoja mmoja, vile vile Taasisi na Kampuni ziweze kuwekeza katika mfumo huu.”

Kwa upande wake Mmoja wa Wakurugenzi wa I Trust Finance Prof. Mohamed Warsame amewataka watanzania kutii sheria ya makatazo ya kutumia ‘Dolar’ kwa baadhi ya huduma badala yake amewataka fedha hizo waweze kuwekeza katika ‘I Dolar’ kwa manufaa Zaidi kutoka na uwekezaji wako.

“Kama mnavyofahamu sheria ya nchi imebadilishwa mwaka huu watanzania hatuwezi kutumia tena ‘dollar’ Watanzania wote, makampuni, mashirika na Taasisi, ata watu binafsi wasiuze kwa kutumia Fedha ya Kigeni ‘Dollar’, inabidi watu wawekeze hizo dola zao kwenye ‘I Dollar’” Prof. Warsame.


Comments