WATENDAJI WA UCHAGUZI TOENI MAFUNZO KWA WASIMAMIZI NGAZI YA KATA: MAPURI


Watendaji wa uchaguzi wametakiwa kutoa mafunzo kwa Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Kata ili kuwawezesha kuratibu na kusimamia uchaguzi ngazi vizuri na kwa weledi.

Hayo yemesemwa leo Julai 23, 2025 Dar es Salaam na Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Balozi Omar Ramadhan Mapuri wakati akifunga mafunzo ya watendaji na wasimamizi wa uchaguzi kutoka mikoa ya Pwani na Dar es Salaam yaliyoanza Julai 21, 2025.

Aidha washiriki wamejifunza namna mbalimbali za kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia katiba, sheria na kanuni za uchaguzi.





Comments