Na: Moses Mashala, @dunialeo, Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Maendeleo ya Vijana Joeli Nanauka amewataka vijana wa Tanzania kuwa wazalendo, wachapakazi wenye nidhamu.
Waziri Nanauka ametoa rai hiyo leo Desemba 23,2025 Jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na Waandishi wa habari kuelezea utekelezaji wa mipango ya Wizara yake katika Serikali ya wamu sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
Aidha amesema kuwa Vijana wanapaswa kuheshimu sheria,walinde amani na mshikamano wa Taifa,na wajitokeze kwa ujasiri kushiriki katika shughuli za maendeleo.
Nakuongeza kuwa "Nawahakikishia vijana wote wa Tanzania kuwa ofisi yangu iko wazi,katika kutoa huduma kwa vijana,tutazingatia falsafa yetu ya kutoa huduma kwa kasi,vituoni kufikika kwa urahisi,

Comments
Post a Comment