Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Albert Chalamila amefanya ziara ya kutembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa barabara ya Mabasi yaendayo Haraka (Mwendokasi) katika barabara ya Bagamoyo Wilaya ya Kinondoni kuanzia eneo la Morocco hadi Tegeta, (BRT 4 LOT 1 & LOT 2)Katika ziara hiyo aliyoifanya Februari 11, 2026 Mheshimiwa Chalamila amesisitiza kuongeza kasi ya utekelezaji wa mradi huo ili uweze kurahisisha na kuboresha utoaji wa huduma za usafiri kwa Wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam.
"Mradi huu wa Mwendokasi ni muhimu sana kwa Mkoa wetu wa Dar es Salaam katika kupunguza msongamano wa magari na kuboresha huduma za usafiri katika jiji hili hivyo ni muhimu kuongeza kasi ya ujenzi ili kuharakisha ujenzi huu," amesema Mhe. Chalamila.
Aidha, Mheshimiwa Chalamila amesema kua miradi yote itekelezwe kwa ubora na ufanisi wa hali ya juu na kwa muda uliopangwa kwani Serikali haitaweza kuvumilia ucheleweshaji wa miradi ya maendeleo pasipokuwa na sababu za msingi.
Comments
Post a Comment