NA. ANGELINA MGANGA.
MWENYEKITI wa Chama cha Mawakili wa Serikali Tanzania (TPBA), Addo Novemba amesema Oktoba 31 mwaka huu kutafanyika mbio maalum za Wakili Marathon katika Jiji la Dodoma, zikiwa na lengo la kuchagiza utoaji wa msaada wa kisheria kwa wananchi pamoja na kuhamasisha ushiriki wa jamii katika michezo.
Amesema marathon hiyo itawakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo Hamza Johari pamoja na mwanariadha nguli Alphonce Simbu ambao wanatarajiwa kushiriki katika tukio hilo.
“Pamoja na kuwa wataalamu wa sheria na kutetea watu mahakamani, hata kwenye mbio pia tupo. Mimi binafsi nimejisajili kukimbia kilomita 21,” amesema Addo Novemba wakati akizungumza kuhusu maandalizi ya marathon hiyo.
Msanii Farid Kubanda naye ameendelea kuinadi marathon hiyo akieleza kuwa ni ya kipekee kwa kuwa itaunganisha msaada wa kisheria, burudani pamoja na michezo ya riadha.
Aidha, wanawake wamehamasishwa kujitokeza kwa wingi kushiriki marathon hiyo, huku waandaaji wakisisitiza kuwa mchezo wa marathon ni msingi wa michezo mingi duniani kutokana na umuhimu wa kukimbia katika maisha ya kila siku na michezo mbalimbali.

Comments
Post a Comment