BIASHARA YETU ILENGE KUSAIDIA JAMII NA KUONGEZA AJIRA: PIUS MAVOA


Mfanyabiashara wa Kituo cha Kuuza Mafuta cha Mavoo Petrol Station kilichopo mkoani Kilimanjaro, Bw. Pius Paulo Mwamvoa, amesema biashara yake inalenga zaidi ya kupata faida, bali pia kushirikiana na jamii na kuchangia maendeleo.

Akizungumza katika mahojiano na Mwandishi wa Dunia Leo, Mwamvoa amewakaribisha wateja kuendelea kutumia huduma za kituo hicho, akisisitiza kuwa biashara hiyo inalenga kujenga uhusiano mzuri na jamii pamoja na kusaidiana katika shughuli mbalimbali za maendeleo.

Amesema moja ya malengo yake ni kuhakikisha biashara inakuwa sehemu ya jamii kwa kutoa fursa za ajira, hususan kwa vijana, huku akieleza kuwa tayari wameanza kutoa nafasi za ajira kwa vijana wa kiume na wa kike.

“Wateja wangu karibuni sana, tutasaidiana mengi. Pia tunaendelea kushirikiana katika maendeleo. Niliamua kuingia kwenye jamii kupitia biashara ili kusaidia kutoa ajira kwa vijana,” alisema Mwamvoa.

Ameongeza kuwa wana mipango ya kupanua shughuli zao za kibiashara, ikiwemo kuendeleza huduma za supermarket na mpango wa kujenga hoteli, huku akisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya wafanyabiashara na jamii.

Kwa mujibu wa Mwamvoa, mshikamano huo ni muhimu wakati wa changamoto au wakati kunapokuwa na jambo la maendeleo linalohitaji ushiriki wa jamii.

Ameendelea kuwataka wananchi na wateja kushirikiana nao katika kuendeleza biashara hiyo, akisema lengo ni kujenga biashara ambayo itanufaisha jamii na kuchangia maendeleo ya eneo hilo. Na. Latifa Botto, Kilimanjaro.

Comments