VIJANA WATAKIWA KUTUMIA FURSA YA UJANA KUTAFITI TAARIFA: SHEIKH REHANI

 

Sheikh Rehani Yasini, Mkuu wa Taaluma katika Chuo cha Al Mustafa International kilichopo Dar es Salaam, amewataka vijana kutumia fursa ya ujana wao kwa kujifunza, kutafuta taarifa sahihi na kufanya tafiti kabla ya kuchukua maamuzi.

Akizungumza wakati wa Matembezi ya Amani ya kumbukizi ya kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w), Sheikh Yasini amesema Mtume Muhammad (s.a.w.w) aliwafundisha waumini kutumia fursa kabla hazijapotea, ikiwemo ujana kabla ya kufikiwa na uzee.

Amesema kijana ana nafasi kubwa ya kunufaika na ujana wake katika nyanja mbalimbali, ikiwemo elimu, kupata taarifa sahihi na kushiriki katika shughuli za maendeleo.

Sheikh Yasini amesisitiza kuwa vijana hawapaswi kuchukua taarifa kwa msukumo au mihemko, bali wanapaswa kuzifanyia utafiti na kuchunguza uhalisia wake kabla ya kuziamini au kuchukua hatua.

Comments